Posts

Image
  “Jana tarehe 12/12/2021 majira ya saa tatu na nusu katika mtaa wa Mabuba jijini Dodoma mbunge Humphrey Polepole alibaini kuvunjiwa dirisha la nyumba anayoishi na kuibiwa flat screen TV moja inch 55 na Specker moja ya Bluetooth, thamani ya mali yote hiyo bado haijaweza kufahamika” Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), Onesmo Lyanga “Uchunguzi wa awali umebaini kuwa mbunge Humphrey Polepole umebaini alisafiri kwenda mkoa wa Manyara katika shughuli zake, upelelezi wenye kuambatana na msako mkali unaendelea ili kuwatafuta wahusika wa tukio hilo na kuwachukulia hatua za kisheria”  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), Onesmo Lyanga “Suala la kwamba ni habari ya siasa sisi hatuoni kwa sababu makazi yamevunjwa kwa hiyo huwezi kusema wahalifu walikuwa wanamtafuta yeye, wangemkuta mwenyewe ishu ingekuwa tofauti ingekuwa ni unyang’anyi wa kutumia silaha au nguvu, bado haieleweki ni lini hasa palivunjwa kwa hi

“Fedha za mkopo zinatumika kwa usafiri na mawasiliano” BOT

Image
  Taarifa ya mwezi ya Maendeleo ya Uchumi inayotolewa kila mwezi na Benki Kuu ya Tanzania yameonesha sehemu kubwa ya fedha zinazokopwa nje hutumika kwa Usafiri na Mawasiliano. 27.2% ya deni ilitumika kwa usafiri Oktoba 2020, kwa Septemba 2021 na Oktoba 23.2% ilitumika kwa usafiri na mawalisiliano. Aidha sehemu inayofuata baada ya usafiri ni ustawi wa jamii na elimu ambayo kwa Oktoba 2021 imetumia 16.2% Sekta ya utalii inawekewa kiwango kidogo zaidi cha fedha zinazokopwa nje ambapo kwa Oktoba 2021 ni 1.0% ya deni la nje ilitumika kwa sekta hiyo.

Baba aliembaka Mwanae anatafutwa

Image
  Jeshi la Polisi Mkoa wa Manyara limesema linamtafuta mkazi wa Kata ya Magugu wilayani Babati, Frednand Yohana ambaye anatuhumiwa kumbaka mtoto wake wa kumzaa mwenye umri wa miaka 11. Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo, Benjamin Kuzaga ameyasema hayo Jumatatu Desemba 13, 2021 mjini Babati wakati akizungumza na waandishi wa habari. Kamanda Kuzaga amesema mkazi huyo wa Magugu alikuwa anambaka mtoto wake wa kike mwenye umri wa miaka 11 (jina lake linahifadhiwa) usiku wakati mke wake na watoto wengine wakiwa wamelala.

Biden atangaza hali ya tahadhari

Image
  Rais wa Marekani Joe Biden ametangaza hali ya tahadhari katika mji ya Kentucky nchini humo, baada ya kukumbwa na mfululizo wa vimbunga vilivyosababisha vifo vya watu sitini huku wengine wengi wakiwa hawajulikani walipo. Vikosi vya uokoaji vimekuwa vikiendelea na zoezi la kuwanasua watu walionasa kwenye vifusi vya majengo yaliyobomolewa na vimbunga hivyo, kwani watu wengi inasemekana bado wamenasa kwenye vifusi hivyo. Biden amesema vimbunga hivyo ni vibaya kuliko vyote vilivyowahi kuikumba Marekani katika siku za hivi karibuni. Habari zaidi kutoka nchini Marekani zinasema watu 70 waliokuwa katika kiwanda kimoja cha mishumaa wanahofiwa kufa, kwani kiwanda hicho kimeharibiwa kabisa.

Meli za mizigo zagongana

Image
  Meli mbili za mizigo ziligongana Kusini mwa Sweden, na kusababisha kupinduka kwa meli moja na mabaharia wawili kuzama baharini, kulingana na mamlaka ya baharini ya Sweden. Ajali hiyo ilitokea majira ya saa 2:30 saa za kimataifa, katika Bahari ya Baltic kati ya ncha ya kusini ya Sweden na kisiwa cha Denmark cha Bornholm kati ya meli ya mizigo ya Uingereza na meli ya Denmark, ambayo ndiyo iliyopinduka, msemaji wa mamlaka hiyo, Carl- Johan Linde ameliambia shirika la habari la AFP Watu kadhaa wanahofiwa kuwa majini na operesheni kubwa ya uokoaji inaendelea, Operesheni kubwa ya uokoaji inayohusisha boti tisa na helikopta inaendelea, katika maji baridi sana, yenye digrii nne tu.